Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kali kwa wale watakaowazomea watu waliovaa nguo zenye rangi ya chama fulani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda Wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa jeshi hilo linachunguza vipande vya video vilivyoonekana kwenye mitandao ya kijamii vikionesha watu wakizomea wenzao kwa sababu wamevaa nguo zenye rangi ya chama fulani.

“Tuna video inayoonesha watu ambao wako sokoni au barabarani wakiwazomea wenzao kwa sababu rangi za nguo zao, kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kama kitaachwa bila kuchukuliwa hatua, kitavunja haki za watu wenginena kusababisha migogoro,” alisema.

Aliwataka wale ambao watazomewa kuripoti kwa mkuu wa polisi katika wilaya husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema walioko wilaya ya Ilala wanaweza kupiga simu kwa kamanda Lucas Mkondya (0715009980), walioko Kinondoni wawasiliane na Kamanda Camillius Wambura (0715009976) na wilaya ya Temeke wampigie Kamanda Andrew Satta (0715009979).

Ni Balaa La kulipiza Kisasi Ama Kuendeleza Uteja
Koeman: Kumuuza Mane Ni Sawa Na Uwendawazimu