Afisa wa Jeshi la polisi nchini Kenya ameburuzwa mahakamani akituhumiwa kumnyanyasa kijinsia na kingono mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa selo.

Taarifa zimeeleza kuwa afisa huyo wa polisi alifanya unyanyasaji huo wa wiki iliyopita katika kituo cha polisi cha Murang’a, ambapo msichana huyo alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kuiba nguo.

Imeelezwa kuwa afisa huyo wa polisi alimuahidi msichana huyo kuwa angempa dhamana kwa makubaliano ya kufanya naye mapenzi.

Askari huyo ambaye ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa siku tano sasa huku upelelezi wa tukio hilo ukiendelea, endapo atapatikana na hatia anaweza kukumbwa na kifungo cha miaka hadi 25 jela.

Tukio hilo limeamsha hisia za wanaharakati na mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo wakililaani vikali.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirikisho la Wanawake Wanasheria nchini humo (Fida), matukio ya unyanyasaji wa kijinsia au kingono wanawake yanayowahusu askari polisi yamekuwa yakiongezeka.

Video: Majambazi wenye mabomu wauawa, Chadema wahoji kila kona sakata la Lissu na Saanane
Timu Lipumba, Timu Maalim Seif waanza ‘Sarakasi’ uchaguzi wa Madiwani