Idara ya Habari ya Klabu ya Polisi Tanzania imetoa taarifa ya maendelel ya wachezaji wa.klabu hiyo waliopata majeraha, kufuatia ajali ya jana Ijumaa (Julai 09) iliyotokea mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Taarifa ya Hassan Juma Mkuu wa Idara hiyo, imeeleza kuwa: Tunamshukuru Mungu hali ya Gerald Mdamu inaendelea vizuri jioni hii baada ya upasuaji uliofanyika usiku wa kuamkia jana wa miguu yote miwili ambayo ilivunjika baada ya timu ya Polisi kupata ajali ikitokea mazoezini na amewekewa pleti.
Mdamu bado amelazwa KCMC akiwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa hospitali hiyo.
Hali za vijana wetu wengine kwa sasa zinaendelea vizuri wamerejea kambimbini baada ya kuruhusiwa Hospitali na watakuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa timu yetu na wa hospitali ya chuo cha Polisi Moshi.
Tunapenda kutoa shukran za dhati kwa Shirikikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Bodi ya Ligi, chama Cha mpira wa miguu Mkoa wa Kilimanjaro, uongozi wa Hospitali ya KCMC pamoja na madaktari wa Hospitali hiyo na wafanyakazi wote na wale wa Hospitali ya Mawenzi, Wafanyakazi wa Kiwanda cha sukari cha TPC, Vyombo vyote vya habari na wadau wake, vilabu vyote vya ligi kuu, familia ya wapenda michezo na wote ambao wamekuwa wakitufariji na kutuombea dua baada ya tukio la ajali tuliyopata timu yetu siku ya Jana.
Hakika kwetu mmetupa faraja kubwa na tunawashukuru kwa moyo wa upendo mliotuonyesha timu yetu.
Hassan Juma
Afisa Habari Polisi Tz
10.07 2021