Imefahamika kuwa Klabu ya Polisi Tanzania imewasilisha ombi la kumsajili kwa Mkopo Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans Heritier Makambo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.
Tayari Disrisha Dogo la Usajili msimu huu 2022/23 limeshafunguliwa tangu Desemba 16 na litafungwa rasmi Januari 15-2023, huku timu zinapaswa kusajili kikanuni ni zile za Ligi Kuu, Championship, First Division na Ligi Kuu ya Wanawake.
Msukumo wa Polisi Tanzania kuwasilisha ombi hilo Young Africans, umetolewa na Kocha Mkuu wa sasa wa Klabu hiyo yenye Maskani yake Makuu mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro Mwinyi Zahera.
Zahera anaamini endapo usajili wa Mshambuliaji huyo utafanikiwa, atakuwa katika mazingira mazuri ya kutatua tatizo la ufungaji kwenye kikosi chake, kwa kuamini Makambo ataweza kufanya kazi hiyo kwa uhakika.
Kocha huyo kutoka DR Congo ndio aliyemsajili Makambo na kumleta Tanzania kwa mara ya kwanza nchini Tanzania akiwa na Young Africans, kabla ya kuuzwa AC Horoya ya Guinea na baadae kusajiliwa tena Jangwani.