Polisi imesema inachunguza Video iliyosambaa Mitandaoni ikionesha watu waliokuwa wakijaribu kumkamata na kumuingiza kwenye Gari Mfanyabiashara Deogratius Tarimo ambaye amesharipoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Gogoni.
Taarifa iliyotolewa kwa Umma na Msemaji wa Jeshi hilo, DCP. David Misime imeeleza kuwa Mfanyabiashara huyo alifika katika Hotel ya Rovenpick, Kiluvya kufanya mazungumzo ya Kibiashara na Watu hao, ambao alikuwa akiwasiliana nao tangu Oktoba 25, 2024.
Jeshi la Polisi kupitia taarifa hiyo limesema litahakikisha linawakamata waliojaribu kufanya tukio hilo kwa ushahidi ambao umeshakusanywa na unaoendelea kukusanywa, ili hatua za Kisheria zichukuliwe.

Maisha: Mbinu zilizonisaidia kudhibiti Mafao yangu
Shambulizi la Israel lauwa 23 Lebanon