Walevi waliojawa na hasira wanadaiwa kuwazidi nguvu Askari wanne wa Jeshi la Polisi nchini Kenya na kuwafungia ndani ya nyumba ya mwanamke anayehusishwa na biashara haramu ya Pombe ya Moshi maarufu kama Chang’aa.

Tukio hilo la kutatanisha, lilitokea katika eneo la makazi duni la King’ong’o viungani vya mji wa Eldoret vilivyopo Kaunti ya Uasin Gishu ambapo maafisa hao walikuwa wakifanya msako dhidi ya pombe haramu.

Inadaiwa kuwa, Walevi hao pia walikuwa wakiwarushia Polisi hao mawe na vitu vingine, wakiwashutumu kwa kulenga eneo lao kila mara pindi wanapotekeleza msako mkali dhidi ya Pombe haramu na ambapo Polisi hao badaye walipata mwanya wa simu na Kikosi cha Polisi cha kupambana na ghasia – GSU, kilifika kutoa msaada.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Uasin Gishu, Benjamin Mwanthi amesema Polisi hao walikaa zaidi ya saa moja katika nyumba ya mwanamke huyo, huku wakikuta zaidi ya lita 300 za pombe haramu kutoka kwa nyumba ya mshukiwa kabla ya kumkamata.

Utengenezaji wa pombe haramu katika eneo hili umechangia pakubwa ukosefu wa usalama na umaskini, kwani Vijana wengi hutumia pesa zao wanazopata katika ujira wa kazi, huku Polisi ikisema kilichotokea ni changamoto ya kiutendaji na zoezi hilo halitaishia hapo bali ni endelevu.

Dkt. Biteko ataka mabadiliko Sheria ya Mtoto kukamilia
Rais Samia kutia neno majadiliano mifumo ya Chakula