Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa linalaani vikali tukio lililosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandishi wa habari wa Wapo Radio aitwaye Sillas Mbise lililotokea August 8, 2018.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Polisi Kanda maalum imeanza kufanya uchunguzi  wa tukio hilo kwa kufungua Jalada la uchunguzi wa picha hiyo ya video iliyosambaa ikimuonyesha Askari akimshambulia mwandishi huyo.

Aidha, Mambosasa amesema kuwa tukio hilo linaenda sambamba na kumtaka mtendewa kuripoti kituo cha polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwakuwa mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko pale ambapo ameona ametendewa kinyume na sheria.

Hata hivyo, Mambosasa ameongeza kuwa jukumu la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao na si kuwapiga wakitenda kosa ambao hawaja kataa kutii amri bila shuruti.

 

Mkuu wa Mkoa agoma kujiuzulu, asubiri maamuzi ya JPM
Mwongozo wa Namna ya Kukabiliana na Kuachishwa Kazi