Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Naibu kamishna wa Polisi, Ramadhan Ng’anzi amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha Waislam wanasherehekea sikukuu ya Eid el Hajj kwa amani na utulivu bila mtu yeyote kumbuguzi mtu.

Amesema kuwa sherehe hiyo ipo kwenye utaratibu wa dini nasi ya kufanyia matukio kama wengi wanavyodhani kuwa nyakati za sikukuu jeshi litakuwa limelala.

Aidha, Kamanda Ng’anzi amewatakia kheri ya sikukuu hiyo Waislam wote huku akiwataka kusherehekea kwa kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi.

“Nawasihi madereva kutovuruga rekodi nzuri ya mkoa wetu kutokuwa na ajali kwa kuendesha magari kwa uangalifu na kutoendesha wakiwa wamelewa na kuwa waangalifu kwa watoto wanaotembea barabarani,” amesema Ng’anzi.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wenye kumbi za starehe kuacha kupiga disco toto na kusema kuwa atakayebainika hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

 

Waamuzi 82 kusimamia sheria 17 Ligi Kuu 2018/19
Amunike atangaza kikosi kitakachoivaa Uganda