Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni linawashikilia watu watano kwa kosa la kuandaa sherehe ya ufuska, kusambaza video inayohamasisha ngono na kusambaza taarifa kinyume na sheria ya makosa ya mtandaoni.

Sherehe hiyo ya ufuska ilipangwa kufanyika Desemba 23, siku 2 kabla ya Sikukuu ya Krismasi ambapo wanaume walialikwa katika sherehe ya kuburudika na wanawake wanaowataka Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa mhudhuriaji alipaswa, kiulikuwa na kadi ya Sh. 150, 000 ambayo mwanaume angepata mwanamke mmoja na na ya Sh. 300,000 inayompa wanawake wawili wa kushiriki nao tendo la ndoa.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi maandalizi ya sherehe hiyo yalipangwa na kutangazwa katika mitandao ya kijamii lakini Jeshi la Polisi wilaya ya Konondoni lilibaini jambo hilo na kuwakamata watu watano akiwamo mwandaaji wa sherehe hiyo.

Akizungumza na gazeti hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema watuhumiwa hao wamekamatwa juzi usiku na bado wanaendelea kuwatafuta wengine waliosambaza video hizo.

“Tumemkamata mwandaaji wa shguli hiyo, tunaye pamoja na wengine wanne walisambaza video hizo, bado tunawatafuta wengine walioisambaza,” amesema Kamanda Kingai.

“Ni kosa kusambaza video inayohamasisha ngono, kusambaza taarifa ile pia ni kinyume na sheria ya makosa ya mtandaoni, hivyo tunaendelea na uchunguzi, utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” ameongeza Kamanda Kingai.

Lwanga amuengua Morrison kikosini Simba SC
Watano Azam FC kuikosa Ruvu Shooting