Polisi wa Oklahoma wamemshikilia kijana mmoja aliyekuwa amejichora michoro mingi ya ajabu usoni iliyofunika sura yake na kumuogopesha mfanyakazi wa kike wa duka kubwa la manunuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, kijana huyo ambaye alitambulika kwa jina la Michael Carter alionekana awali akiwa karibu na mgahawa akiwa amevaa mavazi ya ‘kishetani’ na mask ya dhahabu kwenye jicho lake.

Baada ya muda, kijana huyo alionekana karibu na duka kubwa la manunuzi akiwa na mask nyingine yenye michoro mingi iliyomuogopesha mfanyakazi huyo wa duka. Mfanyakazi huyo alieleza kuwa alijaribu kumuomba aondoke katika eneo hilo lakini mtu huyo alijifungia chooni na kuanza kupiga kelele. Hali iliyomlazimu mfanyakazi huyo kuwaita polisi.

Polisi walipofika katika eneo hilo walimsihi ajitokeze kwa zaidi ya dakika kumi. Baada ya kujitokeza, polisi walibaini mtu huyo alikuwa amejichora michoro mingi usoni, yenye ishara nyingi zilizowahi kutumika duniani, lakini pia ikiwa na jina la Yesu, ‘Jesu Christ’.

Kijana huyo alikamatwa na polisi hao na kufunguliwa kesi ya kuvamia na kumtishia mfanyakazi huyo.

 

Polisi amuua rafiki yake aliyemtembelea nyumbani
Serikali Yanunua Mashine Mpya Ya CT-Scan Muhimbili