Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam
Kamishna wa Polisi Utawala Menejimenti ya Rasilimali watu, CP Suzan Kaganda amewataka askari Polisi wanawake kuchangamkia fursa za elimu, ili kuongeza ujuzi na weledi wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
Kamishna Kaganda ameyasema hayo Septemba 29, 2023 wakati wa kikao na askari Polisi wanawake kilichofanyika katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo amewasilisha kile walichojifunza katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya askari Polisi wanawake – IAWP, uliofanyika nchini New Zealand.
CP Kaganda amewataka askari kujiandaa na chaguzi zijazo kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu ambapo amesema kila askari anapaswa kuzipitia sheria na miongozo ya chaguzi na maswala mengine ya ili kukahakikisha wanatenda haki.
Katika hatua nyingine Kamishna Kaganda amesema dhamira ya amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais wa Jamhuruio ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona idadi kubwa ya viongozi wanawake ndani ya Jeshi la Polisi.
Vilevile amewataka Askari kuendana mabadiliko na matumizi mifumo ya tehama huku aliwataka kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kujiepusha kuingia katika vitendo vya utovu wa nidhamu.
Kwa upande wake Kamshna wa Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Mwamini Rwantale amemshukuru Kamishana Kaganda kwa namna alivyo wasilisha mafunzo yaliyotolewa wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika nchini New Zealand ambapo amebainisha kuwa wasilisho hilo litawajengea uwezo wa utendaji wa kazi za Jeshi hilo kwa askari wanawake.