Ubalozi wa Uingereza na taasisi ya Mercy Coprps Pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam wametoa mafunzo kwa Jeshi la Polisi juu ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii ikiwemo kutumia mawasiliano dharula inapotokea.
Mratibu wa shirika la Mercy Corps Nchini Anthony Sarota amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, hasa upande wa mawasiliano wakai wa dharula.
Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo upande wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Thabitha Makaranga amesema mafunzo hayo yataleta tija na ufanisi katika kukabiliana na majanga ya dharura.
Akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi CP Shabani Hiki amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuwajenga kiutendaji Askari wa Jeshi Polisi.