Jeshi la polisi limezuia ziara isiyo rasmi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam kwa sababu za kiusalama.

Akiongea na waandishi wa habari jijini humo, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa nia ya mgombea huyo kuwatembelea wananchi ni nzuri lakini ziara hiyo isiyo rasmi ina hatarisha usalama na usumbufu usio wa lazima kwa kusababisha msongamano mkubwa katika maeneo anayoyatembelea.

“Wengi wanajitokeza wanashangilia, lakini kwa watu wengine ambao wasio wa makundi hayo, inakuwa inaleta taharuki, hofu,  usumbufu, makelele mengi,  msongamano wa magari,  au hata kusimamisha usafiri katika  eneo hilo ambalo mgombea anakuwepo,” alisema Kamanda Kova.

Kamanda wa polisi akiongea na Edward Lowassa katika eneo la Kariakoo

Kamanda wa polisi akiongea na Edward Lowassa katika eneo la Kariakoo

“Inawezekana huyo mgombea kuna faida anayoipata lakini yeye kupata faida peke yake haitoshi kama suala la usalama halizingatiwi,” aliongeza.

Jana, Lowassa alitembelea soko la Tandale na Tandika jijini Dar es Salaam kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo ambapo umati mkubwa wa watu ulijitokeza.

Ziara hiyo pia ilifika katika eneo la Kariakoo ambapo kutokana na msongamano mkubwa wa watu uliojitokeza, Jeshi la polisi Wilaya ya Ilala lililazimika kumzuia kuingia katika eneo la soko hilo.

Ni Arsenal Vs Spurs Capital One Cup
Henry Ampasha Habari Arsene Wenger