Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad, amewataka Wananchi kuacha tabia ya kutumia Vituo vya Polisi kushitaki kesi za uongo kwa lengo la kukomoana.

Akikagua Mradi wa ujenzi wa Jengo jipya la Kituo cha Polisi Mkoani, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, Hamad amesema wapo baadhi ya watu hutumia Askari wa Jeshi la Polisi wanaowafahamu, kufungua kesi za uongo na kesi za madai jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

Kuhusu suala la maendeleo ya ujenzi, Fundi Mkuu wa ujenzi wa kituo hicho, Omar Khamis amesema wanatarajia kumaliza na kukikabidhi Kituo hicho, baada ya muda wa wiki mbili.

Ujenzi wa Kituo cha Mkoani, umekuja kufuatia kuchakaa kwa Kituo cha Polisi Mkoani ambacho kimerithiwa tokea wakati wa ukoloni na bado kinaendelea kutumika.

Fikiri Elias: Simba SC imetuamsha usingizini
CCM wahimizana kudumisha umoja, mshikamano