Hatimaye Jeshi la Polisi limetolea ufafanuzi amri yake ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini baada ya kutokea mvutano kuhusu uhalali wa kufanyika kwa mkutano mkuu maalum wa CCM, Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani

Jeshi hilo limeubariki mkutano huo na kueleza kuwa marufuku hiyo haihusu mikutano ya ndani ya chama ya kiutendaji na ya kiutawala ambayo ipo kikatiba.

Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani katika mkutano na waandishi wa habari.

“Naomba nirudie hili… hakuna mahala popote ambapo Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya kiutendaji na ya kiutawala inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama vya siasa,” alisema Kamishna Marijani.

CCM imepanga kufanya mkutano mkuu maalum kwa lengo la kumkabidhi uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.

Kumekuwa na mvutano mkubwa na kutolea maneno kati ya UVCCM na BAVICHA katika siku za hivi karibuni kuhusu uhalali wa mkutano huo. BAVICHA waliahidi kwenda mjini Dodoma kusaidia kuzuia mkutano huo huku wakipewa onyo kali na UVCCM.

Kumekucha: Viongozi wa BAVICHA wakamatwa Dodoma
Mambo 5 ya maajabu ya ‘tendo la ndoa’ unayopaswa kuyafahamu 18+