Polisi nchini Kenya wamevamia shule ya kiislamu na kuwakamata waalimu wawili, na kuwaweka chini ya ulinzi takriban watoto 100 kwa kile walichokieleza kuwa ni operesheni ya kukabiliana na ugaidi.

Polisi wamesema kuwa wamechukua hatua hiyo katika shule iliyopo katika eneo la Likoni, kusini mwa mji wa Mombasa baada ya shule hiyo kutuhumiwa kutoa mafunzo ya kigaidi.

“kuna tarkiban wanafunzi 100 na waalimu wanne wa madrasa ambao wamekamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi makao makuu, lakini mpaka sasa hatujaelezwa ni uharifu gani uliofanywa na wanafunzi hawa,”amesema Sheikh Omar

Hata hivyo, polisi wa ndani na wa kigeni wamevamia madrasa hiyo ambapo wanafunzi hao walikuwa wamelala na kuwachukua kwaajili ya upelelezi baada ya kuwepo kwa tuhuma za kutolewa kwa mafunzo ya ugaidi.

Wasira: Katiba mpya imenibeba
Upinzani wagonga mwamba