Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha na Viongozi wa waendesha Pikipiki wamewatembelea wahanga wa ajali za pikipiki na vyombo vingine vya moto katika Hospitali ya Nkoranga Lutheran Hospital iliyopo Arumeru, Mkoani Arusha.

Kikosi hicho, kikiongozwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Solomon Mwangamilo kimefika Hopsitalini hapo kwa lengo la kukusanya taarifa na kutoa pole kwa wahanga wa ajali.

Akiongea Hospitalini hapo, Mwangamilo amesema wameona ni vyema kuwatembelea wahanga hao na kuwapa pole kutokana na majamba ya ajali walizozipata katika mikoa ya kanda ya kasikazini.

Kwa upande wake, Katibu wa waendesha Pikipiki Wilaya wa Arusha, Hakimu Msemo amesema wapo baadhi ya waendesha pikipiki ambao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama Barabarani na kusema wao watakuwa mabalozi wa kufikisha kile walichokiona kwa wahanga wa ajali za pikipiki.

Majaliwa aagiza watumishi kuhamia nyumba za Serikali
Baiskeli chanzo kifo cha Mwandishi Kilimanjaro