Waziri wa Mambo ya ndani ya Uingereza, Suella Braveman ameikashifu idara ya Polisi akidai wamepoa na wameshindwa kukabiliana na waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina.
Braveman amesema Polisi kulinganishwa na makundi mengine ya Waandamanaji kwa kushindwa kutuliza kadhia hiyo ni kuongeza mgogoro wa kisiasa uliosababishwa na vita kati ya Israel na Hamas.
Ameongeza kuwa, idara ya Polisi ya London ilikuwa ikizembea katika kuwajibisha uvunjaji wa sheria unaofanywa na waandamanaji hao wanaoiunga mkono Palestina kiasi hali ya utulivu na tishio la usalama ikawa mashakani.
Aidha, Braveman alisema Waandamanaji hao wanaotaka sitisho la mapigano huko Gaza waejawa na chuki, huku ikiarifiwa kuwa Waziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak anashinikizwa kumfukuza kazi Braveman kwani analeta migawanyiko kwenye kitengo chenye nguvu ndani ya chama tawala cha Kikonsavative.