Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekwama kupata dhamana hivyo ataendelea kukaa rumande katika kituo cha polisi kati.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tumaini Makene ambapo amesema kuwa Mwanasheria huyo amekwama kupata dhamana na kudai kuwa wanasubiri ili kuona kama itawezekana kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au mahakamani.
“Jitihada za kuhakikisha Lissu anapata haki yake ya kisheria ya kupata dhamana zimeshindikana. Hivyo bado yuko polisi tunasubiri utaratibu mwingine wa kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au kufikishwa mahakamani,”amesema Makene
-
Heche awazodoa wasomi, asema uzalendo si kuiunga mkono Serikali
-
Chadema yapata pigo tena, yakimbiwa na madiwani wengine
-
Bombadier yamkaanga Lissu, alala rumande
Hata hivyo, polisi liliongozana na Mwanasheria huyo mpaka nyumbani kwake Tegeta na kwenda kufanya upekuzi kufuata makosa mawili anayoshikiliwa nayo likiwepo kosa la kusema hadharani na kosa la pili ni uchochezi kufuatia taarifa alizozitoa kuhusiana na kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada