Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, limefanikiwa kuwadhibiti majambazi wanne wakiume ambao majina yao bado hayajatambulika, wenye umri kati ya Miaka 30 hadi 35, waliokuwa katika harakati za kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha tarehe.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema majambazo hao walivamia nyumbani kwa Edina Joseph (41), ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa kisasa wakiwa wamevaa Baraka.

Amesema, “Majambazi hao wamefanikiwa kunyang’anya pesa taslim Tzs.1, 100, 000, simu ya samsung moja na simu ndogo tatu baada ya kumtishia kumkata na mapanga ndipo mhanga alipiga kelele za kuomba msaada ambazo silisikika kwa majirani  ambao walifika kwa haraka.”

Kamanda Otieno ameongeza kuwa, “Majirani waliwakuta watu hao ambao walijihami kwa kutaka kuwashambulia askari kwa mapanga na askari pia walifanikiwa kujibu mapigo kwa kuwafyatulia risasi ambazo ziliwajeruhi watuhumiwa hao maeneo mbalimbali ya miili yao.”

Hata hivyo, amesema Majambazi hao wanne walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

Zaidi ya watu Milioni 2 hupoteza maisha kila mwaka - Ndalichako
Kikosi cha RFS chamuondoa Omar Al Bashir Gerezani