Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limezima jaribio la kundi la watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wanaokadiriwa kuwa sita, wakiwa na silaha za jadi nondo na mapanga waliovamia eneo la Kampuni ya Kijiji Park ambalo lipo Kibada, Kigamboni, Temeke linalomilikiwa na Jacob Brounschweiler raia wa Uswisi.

Kwa mujibu wa trifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne imeeleza kuwa, tukio hilo limetokea Novemba 16, 2023, majira ya saa saba usiku ,ambapo Watuhumiwa hao walimfunga kamba mlinzi, kumtishia kumuua kwa nondo na kisha waliingiza gari aina ya Fuso tenki namba T. 307 CNC kisha kuiba mafuta ya Dizel na Petroli.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Jeshi la Polisi baadae lilipata taarifa toka kwa watu wema na kufika haraka eneo la tukio na kumkuta mlinzi akiwa kwenye hali mbaya akaokolewa na baadae wahalifu hao walijaribu kuwashambulia askari ambao walijihami haraka na kuwajeruhi wawili miongoni mwao kwa risasi.

Watuhumiwa hao ambao majina yao hayajafahamika, walipelekwa Hospitali wakiwa na hali mbaya huku mwingine akitambulika kuwa ni Nelson Mbewe (49) mkazi wa Ubungo Kibangu na anahojiwa kwa kina juu ya tuhuma hizo za unyang’anyi wa kutumia silaha huku wengine wakiendelea kusakwa.

Washauriwa kuwajenga Watoto kiimani kuepuka uhalifu
Umeme: REA waanza utekelezaji wa agizo la Serikali