Wananchi Mkoa wa Manyara, wamelipongeza Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuimarisha ulinzi, amani na utulivu wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Babati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wananchi hao wamesema Polisi wamefanikiwa kuthibiti uhalifu na wahalifu, wakati wa kipindi chote cha kukimbiza na kuzima Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2023.
Kwa upande wake Hamad Selemani, ambaye mi Mjasiliamali Mkazi wa Babati ameeleza kuwa amani na utulivu, ndivyo vilivyopelekea wao kufanya shughuli zao za kujiongezea kipato bila kuwa na hofu.
Naye Dereva Bodaboda, Ramadhani Mohamed amesema ulinzi na usalama wa raia na mali zao ulioimarishwa na Jeshi hilo unapaswa kuendelezwa siku zote na usiishie wakati huo pekee kwani umeweza kukuza pato la mtu mmoja mmoja na la Serikali bila mawaa.