Uongozi wa Timu ya Polisi Tanzania inayonolewa na Selemani Matola umesema kuwa wachezaji wake wote leo watapata pesa na zawadi za kutosha endapo wataifunga timu ya Yanga ambayo mlinda mlango wao namba moja ni Metacha Mnata.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa wamejipanga kuona wachezaji wanafurahia ushindi wao mbele ya wapinzani wao Yanga na endapo wakifanikisha kupata ushindi basi watapata walichoahidiwa.

”Tunajua tunacheza na timu ngumu na kubwa jambo lililotufanya tuwaandae wachezai wetu kisaikolojia na wanatambua kwamba kuna zawadi zao ambazo tutawapa wakishinda, “amesema Lukwaro.

Taarifa zisizo rasmi zinaeleza kuwa wachezaji wote wamewekewa mezani dau nono kwa ajili ya kuwapa motisha kuwamaliza wapinzani wao leo.

Polisi Tanzania inacheza leo na Yanga uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wao wa tatu msimu huu. Imeshinda mchezo mmoja mbele ya Coastal Union na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Ruvu Shooting.

Mkuu wa mkoa awacharaza bakora wanafunzi 14 kwa kumiliki simu shuleni
Video: Siri ya Anna Tibaijuka 'kutapika vijisenti vya mboga' yatajwa, Vigogo wapishana kurudisha mabilioni