Jeshi la Polisi wilayani Mvomero Mkoani Morogoro limekiamuru chama cha ACT Wazalendo wilayani humo kusitisha kufanya mikutano yao ya ndani.
Katika barua iliyosainiwa na SSP Julius S. Lukindo ambaye ni Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo imeelezwa kuwa Jeshi la Polisi kwa sasa linashughulikia kesi nyingi za kisiasa hivyo halijakubaliana na ombi la ACT Wazalendo la kufanya mikutano hiyo.
Hata hivyo jeshi la polisi limekishauri chama hicho kusitisha ziara hiyo na kufanya mikutano katika siku za baadae, ambapo jeshi la polisi litakuwa na muda wa kutosha kusimamia shughuli zao.
Agizo hilo ni kufuatia na chama hicho kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma mjini, ZItto Kabwe kuomba kibali cha kufanya muendelezo wa ziara zilizoanza rasmi Februari 19 ambazo zililenga kufanya mikutano, kushiriki kazi za maendeleo na kuzungumza na kamati za maendeleo za kata zao.
-
Wakunga wapinga vikali matukio ya udhalilishaji
-
‘Supermarkets’ zasitisha kuuza nyama toka Afrika Kusini
Aidha mbali na jeshi la polisi kutokukubali kutoa kibali cha ziara hiyo, Mwenyekiti huyo amewahi kushikiliwa na polisi na kutoka kwa dhamana kwa kosa la kufanya ziara hizo za ndani bila kibali maalumu.