Polisi nchini Uturuki imetawanya maadamano ya wapenzi wa jinsia moja yaliyokuwa yanafanyika katika mji wa Instanbul nchini humo.

Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa imefikia hatua hiyo ili kuweza kuondoa uweszekano wa kutokea machafuko ambayo yangeweza kujitokeza kutoka kwa makundi mbalimbali yanayopinga maandamano hayo.

Aidha, wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wamepuuza sababu zilizotajwa na Serikali na kudai kuwa imetumia sababu hizo kwa kutaka kuminya haki na uhuru wa watu hao.

Hata hivyo, wanaharakati hao wamemlaumu Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan kwa kuegemea katika maadili ya Kiislam.

 

China yajitosa rasmi mgogoro wa Afghanistan na Pakistan
Israel yaigeuzia mashambulizi Syria