Kupitia maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili, Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limesema litaendelea na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kuhakikisha wanaibua na kuwachukulia hatua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake (TPF NET) mkoani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Edith Swebe ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Jamii ya kifugaji Namanga Wilayani Longido.

Amesema, “Wakati umefika kwa jamii kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa jamii ambapo Jeshi la Polisi litaendelea kufanya doria pamoja na kutoa elimu kuanzia ngazi ya familia, mtaa, Kata na hata wilaya ili kuhakikisha matukio ya ukatili yanaisha
kabisa.”

Kwa upande wake, Kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Longido akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Boniphace Lugola, amewataka wananchi, viongozi wa vitongoji, vijiji na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwafichua wahalifu katika jamii wanazoishi.

Homepage xcritical Backer's Technical Analysis Toolkit for Crypto
Sheria mpya: Ngono nje ya ndoa jela mwaka mmoja