Polisi imethibitisha msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kushambuliwa kwa mawe walipofika kumuokoa Mama aliyetaka kuuawa na Wananchi akidaiwa kumuua mwanaye wa kumzaa.

Imeeleza kuwa kuna mtu amefariki kwenye uwanja wa mpira, ambapo wananchi wakawa wanahisi Mama yake mzazi amemuua kwa imani za kishirikina hivyo maiti ilipotaka kuzikwa wakakataa wakimtaka Mama yake amfufue

Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na DC Claudia walikuwa maeneo hayo katika ukaguzi wa masuala ya Mwenge na mitihani, waliposikia taarifa za Mama huyo wakapita ili wajiridhishe ndipo Wananchi wakafunga njia na kukazuka vurugu.

Hata hivyo, Polisi imethibitisha kuwa hakuna mtu aliyelazwa isipokuwa vurugu zilikuwa kubwa ila waliokuwa kwenye msafara walijtahidi kujiokoa na Polisi waliwahi kufika eneo la tukio na bado wapo eneo la tukio wakifuatilia kujua waliohusika na vurugu.

Simba yaanza vyema Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara
Simba watarudisha furaha kwa mashabiki wao leo ?