Saa chache baada ya kusambaa taarifa za kufungiwa maisha kwa gazeti la Mawio, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa linawasaka wamiliki na wahariri wa gazeti hilo.

Kamanda wa jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro alieleza kuwa jeshi hilo linawasaka wamiliki wa gazeti hilo pamoja na wahariri ili waweze kusaidia katika uchunguzi unaofanyika kufuatia habari wanazoziandika.

Alisema kuwa gazeti hilo limekuwa likichapisha habari ambazo zimeonekana kuwa za utata hivyo jeshi hilo linawasaka ili waweze kuthibitisha ukweli wa habari hizo.

“Mkuu wa upelelezi analishughulikia suala hilo, bado hawajapatikana lakini wanatafutwa kwa ajili ya kutoa maelezo. Taarifa kamili itatolewa kesho,” Kamanda Siro aliliambia Mwananchi.

Gazeti la Mawio lilifungiwa maisha kuanzia Januari 15 kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Sheria hiyo inampa Mamlaka waziri mwenye dhamana kulifungia gazeti lolote na wakati wowote endapo atajiridhisha kuwa halikwendana na maslahi ya umma.

Chanzo: Mwananchi

 

Video: Lil Wayne awarushia 'microphone' mashabiki walioshindwa kumshangilia
Operesheni Kata Maji yafyeka Nyumbani kwa RPC, Kambi ya Polisi