Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, imeendesha operesheni maalum ya kuwaondoa ombaomba katika jiji hilo, iliyopelekea kuwatupa jela ombaomba 17.

OMBAOMBA Ombaomba

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro jana alieleza kuwa mbali na ombaomba 17 walioswekwa rumande, ombaomba 45 wamekamatwa na kuondolewa katika maeneo hayo.

Alisema kuwa Jeshi hilo linashirikiana na Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa ombaomba hao wanarudishwa walikotoka.

“Kazi hii inaenda vizuri na ombaomba wachache wamebakia ambao wakiwaona askari wanakimbia na kutokomea kusikojulikana,”alisema Sirro.

Operesheni hiyo imefanyika kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwaondoa katikati ya jiji ombaomba wote na kuhakikisha wanarudi walikotoka kwa nauli zao wenyewe.

Zitto: Rais Magufuli ameyapapasa tu majipu haya
Zitto amfagilia tena Magufuli, ampa nyota zilizowashinda Marais Wengi duniani