Kufuatia vifo vya watoto 21 katika eneo la Tavern ya Enyoben Jumapili Juni 26, 2022 familia ya Baba wa Taifa hilo Hayati Nelson Mandela, imetoa wito kwa jumuia za mji huo kupiga Marufuku unywaji wa pombe.
Akizungumza kwa niaba ya Ikulu ya Kifalme ya Mandela hii leo Juni 28, 2022, Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela amesema pombe ni chanzo cha wasiwasi mkubwa kwa wazazi ambao wana wasiwasi juu ya janga la uhalifu wa kijinsia dhidi ya wanawake wakiwemo watoto wachanga, wasichana wadogo na Wazee.
“Pombe inatupiwa sana lawama na watu wengi , inasababisha madhara kwa vijana wetu na zaidi inatela majanga kama haya yaliyotokea ingawa bado tunasubiri ripoti ya Polisi lakini hata ‘abogogo’ (wazee) wapo na wasiwasi katika hili maana kila mtu hayupo salama,” amesema.
Hata hivyo kauli hiyo inakuja wakati tayari baadhi ya sehemu za Starehe zikiwa zimesitisha huduma, ikiwemo baa ya Tavern ya Enyobeni katika Scenery Park ambayo ilikumbwa na mkasa huo wa vifo vya Vijana 21.
Aidha, Mandla Mandela amesema anatoa wito kwa Viongozi wa jamii, mashirika na wote wanaohusika ikiwemo jamii, kuunga mkono marufuku hiyo na kudai kuwa huo ndio wakati sahihi wa kuwakomesha wale wanaoua watoto na kufaidika na maisha ya watu wasio na hatia.
Wakazi katika eneo hilo wanaamini kuwa tavern hiyo katika jamii ina matatizo, huku mke wa mmiliki wa tavern hiyo, Vuyokazi Ndevu akisema inatia wasiwasi na uchungu kwamba watoto walikufa kwenye ukumbi huo.