Ndege ya Shirika la Precision, wikendi iliyopita ilipata hitilafu baada ya kuvamiwa na kundi la ndege aina ya kunguru ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika hilo iliyotolewa leo, ndege hiyo aina ya PW 722 ilikuwa na abiria 68, ilikuwa ikitokea jijini Nairobi nchini Kenya kuelekea jijini Mwanza lakini ilipitia Kilimanjaro.

Shirika hilo limeeleza kuwa rubani wake alilazimika kutumia uzoefu kutua kwa dharura baada ya kubaini kuwa kundi hilo la kunguru limesababisha hitilafu kwenye ndege hiyo.

Kutokana na hali hiyo, ratiba ya ndege za shirika hilo imeathiriwa na kusababisha kuahirishwa kwa baadhi ya safari.

“Wataalam wetu wanafanya tathmini ya ukaguzi ili kushugulikia tatizo lililojitokeza. Mabadiliko ya kusogeza mbele ratiba ya ndege zetu yanatakiwa kufanyika. Tutahakikisha tunaepuka athari za usumbufu wowote kwa wateja wetu ili kufanikisha safari zao,” imeeleza taarifa ya Shirika hilo.

Kundi la kunguru lilikumbwa na nguvu ya ndege na baadhi walinasa kwenye tairi la ndege hiyo na kusababisha changamoto wakati wa kutua. Picha za ndege hiyo zilizosambaa jana zilionesha hali ilivyokuwa.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 11, 2018
Video: Ni hatari sana tusipowabana viongozi wetu- Wakili Manyama