Mshambuliani wa vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Azam FC Prince Dube amejinasibu kuwa tayari kwa mchezo wa mzunguko wa sita dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa kesho Alhamisi Oktoba 15, Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mshambuliaji huyo kutoka Zimbabwe anayeongoza kwa ufungaji mabao tangu msimu wa Ligi Kuu ulipoanza mwezi Septemba, amesema amejiandaa vyema sambamba na wachezaji wenzake kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui FC.

Kuhusu anavyoiona ligi

Kwa mechi za Chamazi nazifurahia kwa sababu nimeshauzoea uwanja na ni rafiki kwa mchezaji yoyote.

Lakini viwanja vya mikoani ni vigumu kwa sababu haviko na usawa mzuri, na kusababisha timu kucheza mipira ya juu muda hivyo ni vigumu kufurahia mchezo mzuri wa pasi za chini.

Pia kuna matumizi makubwa sana ya nguvu.

Kuhusu mchezo ujao

Nimewaona Mwadui kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga hapa Chamazi.

Ni timu nzuri sana, inajua kujilinda kwa nidhamu na kushambulia kwa kasi.

Utakuwa mchezo mgumu kama michezo iliyotangulia.

Hii ni ligi na kila timu inajiandaa vizuri kupata ushindi.

Hata wao wamejianda kama tulivyojiandaa sisi.

Itakuwa mechi ngumu sana. Tunawoamba mashabiki wetu wake kutuunga mkono kwenye mchezo huo muhimu.

Kuhusu mbio za ufungaji bora

Jambo kubwa siyo mimi kufunga bali timu kushinda.

Haitakuwa na maana yoyote mimi kufunga halafu timu haijashinda.

Mara zote timu hutangulizwa mbele kwa sababu ndiyo tunayoipigania.

Ikitokea nikafunga, nitashukuru lakini hata nisipofunga mimi, nitamsaidia mwenzangu yeyote afunge ili timu ishinde kama ambavyo wenzangu wamenisaidia mimi kufunga katika michezo iliyopita.

Katika hatua hii ya ligi ukianza kufikiria ufungaji bora utakuwa unapoteza uelekeo mapema.

Huu ni muda wa kuiwaza mechi ijayo tu, basi…kupata alama tatu na kuisuburi mechi nyingine.

Razak Abalora atua Asante Kotoko ya Ghana
Serikali kuwainua wanawake wanaoishi vijijini