Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube atajiunga na kikosi cha Azam FC kilichoweka kambi kisiwani Unguja – Zanzibar kwa ajili ya kuanza rasmi mazoezi na wenzake chini ya kocha George Lwandamina.

Dube anatarajiwa kuelekea Unguja leo Alhamis (Januari 14), baada ya kufanyiwa vipimo na kuonekana amepona jeraha lake la mkono na yupo tayari kuanza mazoezi.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria amesema idara ya utabibu imemuamuru Dube kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi, baada ya kufanya mazoezi mepesi kwa muda wa siku kadhaa jijini Dar es salaam.

“Vipimo vya Prince Dume vimeonesha yupo vizuri, atakuja kuungana na wenzake hapa unguja wakati tukisubiri majibu ya mwisho yatakavyokua ili kufahamu kama ataweza kurudi uwanjani moja kwa moja kwa ajili ya michezo ya ushindani, lakini kwa sasa yupo vizuri kuanza mazoezi.”

“Tumethibitishiwa na jopo la madaktari kuwa Dube yupo sawa, baada ya kudhihirisha uwezo wake alipokua akifanya mazoezi binafasi Uwanja wa Azam Complex Chamazi, mara baada ya kurejea kutoka Afrika kusini ambapo alifanyiwa upasuaji.” Amesema Thabit

Prince Dube aliumia Novemba 25/2020 akiwa kwenye majukumu ya kuitumikia Azam FC, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans, walioibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na Deus Kaseke, Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Masau Bwire: Tungealikwa Zanzibar, tungetwaa ubingwa
Gwajima ashangazwa na uongo, ufichaji dawa