Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amepata ugeni kwa kumpokea Prince Harry ambaye yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi kwa wadhifa wake kama Rais wa Hifadhi za Afrika kufuatia ziara ya Prince Charles (babake Harry) na mkewe Camilla, ambao walikuwa nchini humo kwa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola mwezi Juni.
Kulingana na taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya Habari, Harry kwa sasa anazuru barani Afrika na kundi la maafisa wa Marekani, wahifadhi na wahisani wakitembelea maeneo tofauti ya wanyamapori na asili.
Harry anafanya kazi na shirika lisilo la kibiashara la African Parks la uhifadhi, ambalo linasimamia mbuga za kitaifa na maeneo yaliyohifadhiwa kwa niaba ya serikali na kwa ushirikiano na jumuiya za mitaa kote barani Afrika.
Serikali ya nchi ya Rwanda ina makubaliano na Hifadhi za Afrika kusimamia mbuga za Akagera na Nyungwe, kwa mkataba wa miaka 20 uliotiwa saini mwaka 2020 ukiruhusu shirika hilo kusimamia Hifadhi ya Kitaifa ya Nyungwe, makazi ya robo ya sokwe barani Afrika wa aina 13 wakiwemo sokwe na tumbili adimu wa Hamlyn na L’Hoest.
Africa Parks pia imekuwa ikisimamia Hifadhi ya Kitaifa ya Akagera, ambayo ni kubwa zaidi nchini na shirika hilo limekuwa mstari wa mbele katika kurejesha hifadhi hiyo ambapo wanyama kama simba na vifaru wamehamishiwa huko.
Shirika hilo, pia linahifadhi mimea zaidi ya 1,000, zaidi ya mamalia 90 na aina 300 za ndege waliorekodiwa, ambao wengi wao hupatikana kwenye mbuga hiyo pekee ambapo pia simamia mbuga 19 za kitaifa katika nchi 11 barani, katika karibu hekta milioni 15, kiasi kikubwa zaidi cha eneo lililohifadhiwa.
Prince Harry, amekuwa akihudumu kama Rais wa Hifadhi za Afrika tangu 2017 na kwa sasa analisaidia shirika hilo kukua kiusimamizi hadi mbuga 30 chini ya usimamizi ifikapo 2030, akiwa ni mwanachama wa tatu wa familia ya kifalme ya Uingereza kuzuru Rwanda katika siku za hivi karibuni.