Kocha mkuu wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana, Prince Owusu ametamba kuchukua point tatu muhimu za mchezo wa kesho ambao utawakutanisha na mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa mzunguuko wa tatu una umuhimu mkubwa kwa wawili hao kutokana na kuwa na hali mbaya kwenye msimamo wa kundi A, la michuano ya kombe la shirikisho.

Prince Owusu  amesisitiza wamekuja kusaka pointi tatu na kutupilia mbali kabisa matokeo ya sare.

Prince Owusu

” Tutafanya kila liwezekanalo kushinda ili kubeba pointi tatu. Tunataka pointi tatu na sio kingine. Wachezaji wote wako fiti.

Kocha Owusu amesema anaifahamu Young Africans kwa sababu alikuwepo hapa mwaka jana kama msaidizi wa kocha Mkuu wa klabu ya Khartoum National, Kwesi Appiah wakati wa mashindano ya Kombe la Kagame na pia ameichunguza zaidi katika DVD nne za mechi za Yanga aluzobahatika kuziona.

” Haitakuwa kazi rahisi kusema tu tutawafunga, Yanga ni timu nzuri lakini tuko tayari kujitoa kwa lolote kuibuka na ushindi. “

Medeama waliwasili jana kwa mafungu wakitokea nchini kwao Ghana, na kufikia katika hoteli ya Protea kabla ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume.

Hii leo wanatarajiwa kufanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa taifa mishale ya jioni.

Medeama wana point moja katika msimamo wa kundi A, kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata baada ya mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia uliochezwa mwishoni mwa mwezi uliopita huku Young African wakiburuza mkia wa kundi hilo kwa kutokua na point, baada ya kufungwa michezo yote miliwi waliyocheza mpaka sasa.

Young Africans walikubali kupoteza dhidi ya Mo Bejaia na kisha TP Mazembe kwa kufungwa bao moja kwa sifuri.

Waziri Charles amsimamisha kazi mtendaji mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula, Charles
Mecky Mexime Asajili Wawili Kagera Sugar