Waziri wa mambo ya nje na Mwenyekiti wa baraza la mawaziri kutoka nchi 16 za SADC, Prof. Paramagamba Kabudi leo Aprili 7 ametaja maazimio waliyokubaliana baada ya kufanya mkutano wa dharura jana juu ya kukabiliana na mripuko wa virusi vya covid -19.
Kabudi amesema baada ya kamati iliyotengenezwa na mawaziri wa afya wa nchi za SADC kukaa,Mawaziri wamekubaliana mabo 12 ambayo yatafanywa na nchi zote kukabiliana na ugonjwa huo.
Akitaja mapendekezo hayo amesema ni ;
- Ufuatiliaji na utekelezaji wa itifaki ya afya kuhusu magonjwa ya mripuko.
- kujiandaa na kukabilia na virusi vya covid -19.
- kubaini wagonjwa, kufuatilia waliokutana na mgonjwa na huduma za tiba.
- uzuiaji na udhibiti wa maambukizi.
- uchunguzi na upimaji wa kumaabala.
- uelemishaji wa madhara na ushilikiswaji wa jamii.
- hatua stahiki za afya ya jamii.
- uratibu wa kikanda wa kukabiliana na virusi vya covid 19.
- uwezeshaji na usafirishaji wa bidhaa muhimu miongoni mwa nchi za SADC wakati wa mlipuko wa virusi vya covid-19.
- Covid -19 na uwezeshaji wa kibiashara.
- Covid -19 na masuala ya udhibiti wa biashara katika ukanda.
- usimamizi wa majanga hatarishi katika ukanda wa SADC.
Prof. kabudi amesema mapendekezo hayo ndiyo mikakati ya kudhibiti athari na kuenea kwa ugonjwa huo ambapo kwa upande wa nchi za SADC 16, tayari nchi 14 zimeathirika, watu 2127 wameathirika na vifo 38.
” Muongozo huu utawezesha usafirishaji wa bidahaa muhimu, na bidhaa muhimu zimeainishwa katika muongozo huo kuwa ni chakula, vifaa vya tiba , dawa ikiwa ni pamoja na vifaa vya mtu kujikinga asipate maradhi hayo, mafuta ikiwa ni pamoja na mkaa wa mawe” Amebainisha prof. Kabudi
Aidha amesema wananchi wametakiwa kuendelea kufuata miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya juu ya kujikinga na virusi vya covid -19.