Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale.
Prof. Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo.
Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu, ili wazungumzie suala la Katiba Mpya.
Hata hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na mwisho mzuri