Waziri wa katiba na sheria, Profesa Palamagamba Kabudi jana amewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho mbalimbali wa mwaka 2017.
Ambapo amesema Serikali imeufuta Wakala wa ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), na kuhamishia majukumu yote yaliyokuwa yakitekelezwa na TMAA kwenye kamisheni ya Madini, ambayo itaanzishwa hivi karibuni.
Amesema kamisheni hiyo ambayo imependekezwa itakuwa na makamishina tisa watatu kati yao akiwemo mwenyekiti, watakuwa wa kudumu na watashirikiana na mtendaji mkuu kutekeleza majukumu ya kilia siku.
-
Halima Mdee Akamatwa, Atupwa Selo
-
Video: Acacia yatafuta suluhu Marekani, Wapiga dili wamzuia JPM kwenda nje
-
Lipumba atangaza mkakati wa CUF kusaidia kukomesha mauaji Kibiti
Hata hivyo ameongeza kuwa kupitia marekebisho hayo, vyombo mbalimbali vitaanzishwa ambavyo vitahusika katika shughuli za madini kwa niaba ya serikali, ikiwemo kuanzisha hifadhi ya dhahabu na vito chini ya Benki kuu ya Tanzania (BOT), maghala ya serikali kuhifadhia madini
Pamoja na kuimarisha mfumo wa udhibiti na usimamizi wa shughuli za uzalishaji, usafirishaji wa madini na bidhaa nyingine zitokanazo na madini katika maeneo ya migodi na kuzuia uuzwaji na usafirishwaji wa madini ambayo hayajaongezewa thamani.