Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Profesa Godius Kahyarara amesema licha ya serikali kutopanga bei, hata wafanyabiashara hawaruhusiwi kupanga bei.
Katika taarifa ya Profesa Kahyarara amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kwa mujibu washeria zinazosimamiwa na serikali katika kulinda maslahi ya wadau wa soko.
Amesema sheria ya ushindani ndiyo sheria mama inayotumika kudhibiti vitendo vya namna hiyo.
Alitaja kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Ushindani Na. 8 ya 2003 kinazuia makubaliano ambayo malengo, matokeo au matokeo tarajiwa yake ni washindani (a) kupanga bei (b) kufanya mgomo (c) kukubaliana katika manunuzi, na (d) kuzuia uzalishaji.
Aidha, kutokana na Kifungu hicho, alieleza sheria zingine zote za mambo ya udhibiti katika soko zimerejea Sheria ya Ushindani kushughulikia mambo ya ushindani nchini.