Katibu Mkuu (Sera na Uratibu), Prof. Faustin Kamuzora amefanya ukaguzi katika kituo cha operesheni ya mawasiliano ya dharura na kujua maendeleo ya kituo hicho kilichopo Ofisi ya kanda Maalumu ya Jeshi la Zima moto Jijini Dar es salaam.

Akitoa maelezo ya jinsi mradi huo unavyofanya kazi, Mratibu wa Taifa wa Mradi huo, Alfei Daniel amesema kuwa Mradi huo unafuatilia dharura za maafa nchini ikiwemo Ukame na Mafuriko.

Amesema kuwa mradi huo una vituo 36 tofauti tofauti nchini ambavyo vina wawezesha kupata taarifa popote walipo kupitia mtandao maalumu,

“Mfumo ambao umefungwa unaweza kutabiri na kutoa taarifa za maafa zinazoweza kutokea popote katika vituo hivyo kwa kutumia mtandao, kwa mfano kujaa kwa maji ambako kunaweza kupelekea mafuriko,” amesema Alfei

Kwa upande wake, Prof. Kamuzora ameshauri mradi huo ufanye jitihada kutoa elimu ya uokoaji kwa wanafunzi mashuleni na raia wote kwa ujumla,

Hata hivyo, mradi huo wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali ulianza rasmi mwezi Januari, 2017 kwa dhumuni hasa la kuwezesha mawasiliano ya kujitahadhari na maafa,

 

Video: Uhamiaji yaelezea faida za Hati za kusafiria za 'Kielektroniki'
Mahakama kuingia katika mfumo wa kielektroniki