Aliyekuwa Mshauri Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM.

Katika taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM, mkoa wa Singida, Martha Mlata imetuma salamu za kumkaribisha Katibu huyo wa Wizara ya Maji na kumtaka kuunganisha nguvu ili kuweza kukiimarisha chama katika ngazi ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Aidha, hivi karibuni Prof. Kitila Mkumbo alitangaza kujivua uanachama wa ACT Wazalendo akisema kuwa kitendo cha kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo na kuwa Katibu Mkuu wa Wizara kuna mgongano wa kimaslahi, hivyo ni bora akashikilia upande mmoja.

“Kwa niaba ya CCM mkoa wa Singida, namkaribisha Prof. Kitila Mkumbo kwa mikono miwili tuendelee kuimarisha chama cha mapinduzi katika mkoa wetu na taifa kwa ujumla, pia katika kusimamia na kuitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ustawi wa mkoa wetu na taifa letu,”amesema Martha Mlata

Video: Mugabe alitunishia jeshi msuli, Nyumba Lugumi kunadiwa upya
Rais Mugabe agoma kung'oka madarakani