Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amekitaka chama cha mapinduzi CCM kuacha kupandikiza usaliti ndani ya chama chao.

Ameyasema hayo alipokuwa akimnadi mgombea wao wa udiwani, Abubakar Safi Kondo kwenye Kata ya Nachingwea Wilaya Ruangwa Mkoani Lindi, ambapo amesema kuwa kitendo cha CCM kupandikiza usaliti ndani ya chama chao hakikubariki.

Amewataka wapiga kura wilayani humo kupeleka salamu kwa CCM kuwa kitendo chao cha kumshawishi diwani wao kuwasaliti na kujiunga na chama hicho ambacho kimemteua kugombea kwenye kata hiyo kimegonga mwamba.

“Lazima tulete mabadiliko, CCM wameshindwa kutekeleza haki ya wananchi wa kusini, tupate fursa kuhakikisha hizi mbinu ambazo walizifanya za diwani wetu kutusaliti tuwarudishie salamu watu wa CCM hatukubali kusalitiwa,”amesema Prof. Lipumba

Aidha, amesema kuwa anamkubali Rais Dkt. John Magufuli kwa mpango wake wa kupambana na rushwa, lakini kitendo cha CCM kurubuni madiwani nacho ni rushwa jambo ambalo hakubaliani nalo.

Hata hivyo, upande wa chama cha CUF unaomuunga mkono, Prof. Lipumba wanashiriki uchaguzi uliotangazwa na Tume ya Taifa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, huku upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu Maalim Seif ukiwa na msimamo wa kutoshiriki.

 

 

Mbunge ataja vijiji vyenye majina ya sehemu za siri Bungeni
Video: Kangi Lugola akijitahidi ataweza kuvaa viatu vya enzi zangu- Mrema