Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshinda pingamizi dhidi ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini na watu wake katika kesi ya bodi ya Udhamini – RITA.

Mahakama Kuu mbele ya Jaji, Wilfred Dyansobera imetoa maamuzi juu ya mapingamizi yaliyowekwa na Lipumba aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili, Mashaka Ngole na Majura Magafu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Shauri (Namba Miscilleneous Civil Application No. 51/2017) kuhusu CUF kuomba kuwazuia Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa na Lipumba wasifanye kazi ya Bodi hiyo mpaka pale shauri la msingi Namba 13/2017 litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu.

Aidha, Jaji Wilfred ameyatupilia mbali mapingamizi hayo kutokana na kutokuwa na hoja za msingi za kisheria na kukubaliana na hoja zilizowasilishwa na Mawakili upande wa CUF unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho akiwepo, Fatma Karume.  

Hata hivyo, hoja za pande zote mbili zitawasilishwa kwa maandishi kwa utaratibu Oktoba 19, 2017 na Ally Salehe ambaye ni muombaji anapaswa kuwa amewasilisha huku Oktoba 17, 2017 upande wa walalamikiwa wanapaswa kuwa wamejibu.

Kane aipeleka Uingereza kombe la dunia
Magazeti yaTanzania leo Oktoba 6, 2017