Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imelaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha  vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hayo yamesemwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema maelfu ya mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa ikiingizwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia 47.2 ya maji yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa

Mbali na mifugo  hiyo, Waziri Maghembe amesema kuwa maelfu ya Matrekta ya kutoka nchini Kenya yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na Serengeti

Kufuatia hali hiyo, Waziri Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye  mifugo  Loliondo warudi makwao mara moja, Mkoa na Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja

Kwa upande wa Utalii, Ameziagiza kampuni zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya biashara kwa mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba, Ikiwa pamoja na kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na Serikali pamoja kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi.

 

Mourinho Aigwaya PL, Ageukia EFL Cup, FA Cup
Liverpool Wamvutia Kasi Adam David Lallana