Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa kujenga Gati za Bandari ya Bukoba na Kemondo, unaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 40, kukamilisha mradi huo ifikapo Mei 2024.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo katiaa ziara yake Mkoani Kagera ya kukagua miradi mbalimbali ambapo amesema mradi wa Bandari ya Bukoba unafanyiwa maboresho ikiwemo kujengwa gati jipya, kuboresha magati yaliyopo, ujenzi wa jengo la abiria, ujenzi wa maegesho ya magari, ujenzi wa miundombinu ya umeme na maji ya mvua itakayogharimu Sh Bilioni19.54 na Kemondo Bilioni 20.39.

Amesema fedha hizo ni za kazi nne moja na kujenga magati mawili, kukarabati jengo la Abiria la VIP, kuongeza kina cha maji ili meli ziweze kuingia vizuri na katika jiji la Mwanza tayari Serikali inaendelea na ujenzi wa Meli kubwa ya MV Mwanza yenye urefu wa mita 92.6 ambayo inatarajiwa kumalizika Mei 2024.

Kwa Upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu mamLaka ya usimamizi wa Bandari Nchini, Juma Kijavala amesema mategemeo ya mradi wa Kemondo ni kukamilika kukamilisha mradi huo Machi 2024, ili Bandari ya Kemondo na Bukoba ziweze kufanya kazi kwa wakati.

Awali akizungumza katika eneo hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkuu wa Wialaya Misenyi Kanali Willison Sakulo amesema wanaishukuru Serikali kwa kufanya Maboresho na maendeleo ndani ya Mkoa huo kwani kukamilika kwake kutaongeza fusra za ajira.

Rais Samia atengua uteuzi wa Naibu Waziri
Wasiowajibika kwa Wananchi wakataliwa CCM