Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuhakikisha lina ainisha gharama za Ujenzi wa miradi mbalimbali badala ya kutegemea makadilio ya Wakandarasi wanapotekeleza miradi.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akifungua Semina ya Wadau wa Ujenzi iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi ambapo amesema kutokana na utaratibu mbovu uliopo hivi sasa Watanzania wanatumia hata vifaa visivyokuwa na ubora wowote.
“Sekta ya ujenzi ina mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa na huwezesha utekelezaji wa miundombinu mbalimbali kuimarika na kuwa kichocheo kikubwa kwa sekta nyingine za kiuchumi ikiwe kilimo,utalii nishati na viwanda,” amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Mayunga Nkunya amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa changamoto zote zilizopo kwenye sekta hiyo zitajadiliwa katika Semina hiyo na kupatiwa ufumbuzi ili kuepusha hasara na athari ambazo zinaweza kulikumba Taifa endapo hatua hazitachukuliwa.
- Wivu wamponza mke atiwa mbaroni
- Mwanachuo akamatwa kwa kumiliki bastola
- Mpina atoa maagizo kiwanda cha Azania
Hata hivyo, ameongeza kuwa kutokana na kukosekana kwa Ushirikiano kutoka kwa wadau wa Ujenzi ndio sababu za changamoto hizo kujitokeza hivyo kupitia mkutano huo anaamini watafungua sura mpya ya maendeleo katika sekta hiyo na taifa kwa ujumla