Katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya kikamilifu mapato yake yatokanayo na vyanzo mbalimbali, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewataka wamiliki wa Meli na Majahazi wanaosafirisha mizigo kati ya Tanzania Bara na Visiwani kulipa malimbikizo yao kabla hawajachukuliwa hatua.
Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es salaam na kutembelea eneo la kuhudumia mizigo ya Pemba, Unguja, Mafia na Comorro na kujionea hali halisi jinsi shughuli zinavyoendeshwa.
“Orodha ya majina tunayo ila nawaagiza muwape taarifa rafiki zenu ambao wanadaiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwamba mpaka kufikia mwisho wamwezi huu wawe wameshalipa, vinginevyo meli zao zitazuiliwa baharini,”amesema Prof. Mbarawa.
-
TCAA yapiga marufuku kununua, kurusha ‘drones’ bila kibali maalum
-
Prof. Maghembe aapa kula sahani moja na majangili
-
JPM amteua Prof.Luoga kuwa mwenyekiti TRA
Aidha, katika hatua nyingi Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA kuziba mianya yote ya ukwepaji kodi bandarini hapo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi bilioni moja kwa mwezi.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kama TPA itasimamia vizuri bandari hiyi kwa kuziba mianya yote ya ukwepaji kodi na kuwadhibiti baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakipitisha bidhaa kwa njia za panya, basindari hiyo itakuwa mfano wa kuigwa.