Katika kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania inaimarika na kuwa katika kiwango cha juu cha ushindani, Wakufunzi wote nchini wametakiwa kutumia lugha zinazosaidia wanachuo kuwajengea udilifu badala ya kuwakatisha tamaa kwa maneno ambayo yanawavunja moyo wa kuendelea kujifunza na kubadili tabia zao endapo zinakuwa hazina tija katika maendeleo yao ya kitaaluma.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawara wakati wa ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo Cha Reli kilichopo Tabora.
Amesema kuwa lazima wakufunzi watambue wapo pale kwa ajili ya wanachuo kwani wasingekuwepo nao wasingekuwa na kazi ya kufanya kazi katika vyuo hivyo watimize wajibu wao wa kuwajenga wanavyuo kisaikolojia.
Aidha, Prof. Mbawara ameongeza kuwa Mkufunzi Mzuri ni yule anapoona maendeleo ya mwanachuo wake hayaridhishi ni jukumu lake la kukaa naye na kumsikiliza na kisha kumshauri njia nzuri ya kumuondoa pale alipo na kwenda mbele zaidi.
-
Tazama hapa matokeo kidato cha sita (ACSEE), ualimu (DSEE) na GATCE 2017
-
Zifahamu Shule kumi zilizofanya vizuri matokeo ya kidato cha sita
-
Kigwangalla aagiza kuboresha huduma za afya Wilaya ya Tunduru
Hata hivyo, amewataka wanafunzi kuwa waadilifu na kusoma kwa bidii na kuongeza kuwa uadilifu huanzia katika shule na sio kazini hivyo wawe waadilifu kwa kutimiza kile mabacho kimewapeleka chuoni hapo.