Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amezitaka Mamlaka za Maji nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kujiendesha kibiashara ili kuachana na zana ya kutegemea fedha au ruzuku kutoka Wizarani.
Hayo yamesemwa mkoani Singida na Waziri Maji, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maji inayosimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA).
Amesema kuwa mamlaka zinatakiwa zibadilike zifanye kazi kibiashara, ziongeze mindao ya maji kwa wananchi ili wananchi wapate majisafi na salama na zenyewe zijiongezee makusanyo.
“Katika kipindi changu biashara ya kutegemea kupata asilimia 25 ili kulipia gharama za uendeshaji haipo, Uadilifu ni jambo muhimu sana, heshima inapanda na mambo yanakuwa mazuri endapo mtakuwa waadilifu” amesema Waziri.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskasi Muragili amemshukuru Waziri kwa kufanya ziara Singida ya kukagua miradi ya Maji na kukionea changamoto zilizopo katika mkoa huo.
-
Mswada wa sheria ya vyama vya siasa wawakosha wabunge CCM
-
Mkuu wa Majeshi ateta na Kamati ya Ulinzi na Usalama Njombe
-
DC Msafiri ashiriki Ibada ya kuuombea mkoa wa Njombe