Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imepanga kuwapatia ruzuku wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza mchango wa madini katika pato la taifa kutoka asilimia 3.5 ya sasa hadi 10.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha Tunatekeleza kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Taifa(TBC).
“Sekta ya Madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa,lakini dhamira yetu ni kwamba wakati tunaingia kuwa nchi ya kipato cha kati madini yanapaswa kuchangia si chini ya asilimia kumi”

Aidha aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, hivyo adhma ya Wizara yake ni kuongeza kasi ya pato linalotokana na sekta ya madini na
Aliongeza kuwa ili mafanikio hayo yafikiwe Serikali imekusudia kupandisha hadhi ya wachimbaji wadogo ili wafikie ngazi ya kuwa wachimbaji wa kati na hivyo sekta hii itachangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa.
Aidha Waziri Muhongo alisema kuwa Serikali imepokea pesa mkopo wa Tsh. Bilioni 3 kutoka Benki ya Dunia na imepanga kutoa ruzuku ya vifaa kwa wachimbaji hao wakati wowote kuanzia sasa.
“Serikali imeshaanza kutoa maeneo na kufikia tarehe 15 septemba tutaanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji hao” alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuzuia utoroshaji wa madini nje ya nchi Profesa Muhongo alisema kuwa tangu mwaka 2012 Wizara yake iliweka madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Kilimanjaro na Mwanza na wakafanikiwa kukamata madini zaidi ya tani kumi.

Jaffo Asema Serikali Itaendelea Kugawa Maeneo Kwa Kuzingatia Katiba na Sheria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli Atoa Siku Saba kwa Wizara ya Ujenzi Kulipa Deni Wanalodaiwa na NHC